Home news KISA MAYELE…BARNABAS AIBUKA NA HILI…AGUSIA ISHU YA WAZAWA…

KISA MAYELE…BARNABAS AIBUKA NA HILI…AGUSIA ISHU YA WAZAWA…


WAKATI wachezaji wazawa wakionekana kung’ara msimu huu katika orodha ya wafungaji mabao, nyota na kocha wa zamani wa Mtibwa Sugar, Vicente Barnabas ametoa angalizo kwao huku akimtaja staa wa Yanga, Fiston Mayele kuwa atawatibua.

Kwa misimu kadhaa nyuma, imeshuhudiwa wachezaji wa kigeni waking’ara katika ufungaji bora lakini msimu huu wazawa wameonekana kufunika hadi sasa kuliko wanaocheza soka la kulipwa hapa nchini.

Hadi sasa kati ya wachezaji watano wanaoongoza kwenye ufungaji, wanne ni wazawa, huku mmoja pekee, Mayele akipenya kwa kuwa na idadi ya mabao matano na kufanya vita kuwa ngumu katika kuwania tuzo ya mfungaji bora.

Wachezaji hao ni Jeremiah Juma (Tanzania Prisons) ambaye pia ni mchezaji pekee aliyefunga hat-trick kwenye Ligi Kuu msimu huu, Vitalis Mayanga (Polisi Tanzania), George Mpole (Geita Gold) na Reliant Lusajo wa Namungo.

Akizungumza na jijini hapa, Barnabas alisema kung’ara kwa wachezaji wazawa ni kutokana na kutambua thamani yao na kuwa na wivu wa mafanikio katika soka.

Alisema pamoja na kuanza vyema msimu, lakini ni mapema kuwatabiria makubwa zaidi kwani ligi haijafika hata nusu huku ikiwa na ushindani na kwamba hawapaswi kubweteka kwani kasi ya Mayele siyo ya mchezo.

“Kwa sasa ni mapema kutabiri kwa sababu tunaona kasi ya ligi ilivyo, lakini unaona kasi ya Mayele na timu yake, lazima wawe makini wanapopata nafasi, inawezekana mfungaji bora asitoke hata Simba na Yanga, kimsingi ni kuendelea kupambana,” alisema.

Kwa upande wake straika wa Geita Gold, George Mpole alisema matamanio yake msimu huu ni kuandika historia ya kuwa mfungaji bora huku akibainisha kuwa anafahamu kazi sio ndogo. “Tuna-jua ushindani ni mkali lakini ni kupambana kuhakikisha msimu huu nafikia malengo. Naitamani sana nafasi ya ufungaji bora na pia kuisaidia timu yangu kuwa matokeo mazuri,” alisema.

SOMA NA HII  HAYA HAPA MAAGIZO YA MO KWA KOCHA DIDIER GOMES