Home news HII YANGA YA GSM NI NOMAA..YATUMIA 50MIL KUIPORA SIMBA STRAIKA…APEWA MKATABA ‘KUFRU’…

HII YANGA YA GSM NI NOMAA..YATUMIA 50MIL KUIPORA SIMBA STRAIKA…APEWA MKATABA ‘KUFRU’…


IMEFAHAMIKA kuwa uongozi wa Yanga umetumia Sh 50Mil kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa Mbeya Kwanza, Chrispin Ngushi aliyekuwa akiwindwa pia na Simba na kumpa mkataba wa miaka mitatu.

Usajili wa Ngushi mwenye mabao matatu akicheza michezo 11 ya Ligi Kuu Bara msimu huu, ni wa nne kwa Yanga kusajiliwa kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo uliofunguliwa Desemba 16, 2021.

Wachezaji wengine waliosajiliwa na Yanga na kutambulishwa ni Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ kutoka Azam FC, Denis Nkane (Biashara United) na Aboutwalib Mshery (Mtibwa Sugar).


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, mshambuliaji huyo amesajiliwa kwa dau hilo baada ya pande zote mbili za Yanga na Mbeya Kwanza kufikia muafaka mzuri.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, katika makubaliano hayo, ni lazima asaini mkataba wa miaka mitatu kutokana na umri wake mdogo aliokuwa nao utakaomfanya adumu muda mrefu katika soka.

Aliongeza kuwa, dau hilo la usajili litakwenda sambamba na mshahara wa Sh 3Mil kwa kila mwezi kwa kipindi chote atakachokuwepo Yanga pamoja na kukaa katika apartment nzuri ya kisasa.

“Haikuwa Mkazi rahisi kufanikisha saini ya Ngushi kutoka Mbeya Kwanza kuja Yanga, kwani kulikuwepo na vita kubwa kutoka kwa wapinzani wetu (Simba) ambao walikuwa wakihitaji saini yake.

“Usajili wake tulifanikisha wiki moja iliyopita kabla ya jana (juzi) kumtambulisha rasmi kwa kuachia picha zake zikimuonesha akisaini mkataba na Yanga.

“Kama uongozi tulifkia  uamuzi wa kumpatia ada ya uhamisho ya Sh 50Mil pamoja na mshahara wa Sh 3Mil kwa kila mwezi sambamba na apartment ambazo tumekuwa tukiwapa wachezaji wetu wa kigeni na wale wanaotoka nje ya Dar,” alisema mtoa taarifa huyo.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alipotafutwa kuzungumzia hilo, alisema: “Dau la usajili ni siri kati ya uongozi wa timu na mchezaji husika, hivyo sitaweza kuzungumzia hilo.”

SOMA NA HII  MASTAA AZAM FC WAMUAMULIA KOCHA WAO...WAPANGA KUMFANYIA 'NDOMBOLO'...AFUKUZWE..