Home Uncategorized NJOMBE MJI HUKO MAMBO SIO MAMBO

NJOMBE MJI HUKO MAMBO SIO MAMBO

EDGER Mtitu aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa timu ya Njombe Mji amebwaga manyanga kwa kile alichoeleza ni kutokuwa na maelewano na viongozi wenzake ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Njombe Mji ipo kundi  A imecheza mechi 11 inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 16 kinara ni Dodoma FC yenye pointi 24 kibindoni.

Taarifa zinaeleza kuwa mwenendo mbovu wa timu hiyo ambayo ilishiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 ni moja ya sababu iliyochangia kujiuzulu kwa kiongozi huyo.
SOMA NA HII  BOCCO BALAA LAKE JANA LILIKUWA KWA MTINDO HUU