Home Uncategorized MWADUI FC YAPANIA KUTIBUA REKODI YA YANGA

MWADUI FC YAPANIA KUTIBUA REKODI YA YANGA


KHALID Adam, Kocha Mkuu wa Mwadui FC amesema kuwa leo watapambana kutibua rekodi ya Yanga iliyowekwa kwenye mechi 14 ya kucheza bila kufungwa ndani ya Ligi Kuu Bara.


Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze itashuka Uwanja wa Kambarage, leo Desemba 12 kusaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC ambayo imekuwa na mwendo wa kusuasua.


Ikiwa imecheza jumla ya mechi 14 ndani ya ligi imeshinda mechi tatu na kupoteza jumla ya mechi 10 na imepata sare moja pekee.

Inakutana na Yanga ambayo imeshinda jumla ya mechi 10 na sare nne kwa msimu wa 2020/21 ndani ya ligi ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 34.

Adam amesema:”Tunawaheshimu Yanga ila tunaamini kwamba tutashinda mchezo wetu ili kutibua rekodi yao ya kucheza bila kufungwa.


“Kikosi chetu hakijawa na mwendo mzuri hivyo ili tuweze kurejea kwenye ubora ni lazima tupate matokeo mbele ya timu inayofanya vizuri hilo linawezekana mashabiki watupe sapoti,” .


Mwadu FC ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 10 kibindoni baada ya kucheza mechi 14 ndani ya Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  YANGA YATOA MSIMAMO KWA CARLINHOS