Home news TAIFA STARS YAREJEA DAR IKITOKEA BENIN

TAIFA STARS YAREJEA DAR IKITOKEA BENIN


TIMU ya taifa ya Tanzania,  Taifa Stars imewasili leo Oktoba 11 ikitokea nchini Benin ambapo ilikuwa na mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Stars jana ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0  dhidi ya Benin na kukusanya pointi tatu kibindoni.

Ushindi huo imeupata ikiwa ni siku tano zimepita baada ya kulala kwa kuchapwa bao 1-0 Uwanja wa Mkapa.

Ni bao la Simon Msuva ambaye alipachika bao la ushindi dakika ya 6 na kuifanya Stars kuwa namba moja katika kundi J ikiwa na pointi 7 sawa na Benin iliyonafasi ya pili.

Msuva amesema kuwa ushindi ni zawadi kwa Watanzania.

SOMA NA HII  UKWELI MCHUNGU...KWA YANGA HII YA LEO..SIMBA WAPEWE MAUA YAKE TU MAPEMA...