KATIBU Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Omar Hassan King, amesema Ligi kuu Zanzibar, itachezwa katika kituo kimoja cha Unguja ili kupunguza timu kusafiri pamoja na gharama nyingine za uendeshaji timu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, ameeleza kwamba, Serikali imefikia uamuzi huo kwa lengo la kujikinga na virusi vya Corona.
Ameongeza kuwa katika ligi hiyo hakutakuwa na mashabiki watakaoruhusiwa kuingia uwanjani ili kuchukua tahadhari zaidi ya janga la Corona.
Viwanja viwili vitatumika kwenye mechi zote zilizobaki ikiwa ni Uwanja wa Aman na Mau. Ligi ya Zanzibar ilisimamishwa tangu Machi 17.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.