Home Azam FC KOCHA AZAM ALIA NA VIWANJA BONGO

KOCHA AZAM ALIA NA VIWANJA BONGO



KOCHA mkuu wa Azam, George Lwandamina amefunguka kuwa ubovu wa miundombinu ya viwanja hapa nchini unachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha mchezo wa soka.

Azam ambayo haijapata ushindi tangu Desema 31, mwaka jana, juzi Alhamisi, ilikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Coastal Union mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Akizungumzia sababu ya matokeo yasiyoridhisha kwenye kikosi chake kocha Lwandamina amesema kuwa ubovu wa
viwanja ni changamoto kubwa inayosababisha timu nyingi kushindwa kucheza mpira wa burudani au soka la pasi.

“Miundombinu ya viwanja kwenye mchezo wa soka ni miongoni mwa vitu vya muhimu katika ukuaji wa mchezo huu duniani.

“Hii ni kwa sababu ili uweze kucheza mpira wa pasi nyingi, na burudani unahitaji mazingira ya uwanja unaoruhusu hali hiyo, kama itashindikana basi unakuwa kwenye wakati mgumu.

“Kwa mfano sisi Alhamisi tulipoteza mchezo wetu dhidi ya Coastal, matokeo ambayo yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na ubora wa uwanja wa Mkwakwani ambao ulishindwa kuturuhusu kucheza  mpira wa pasi za chini.



SOMA NA HII  AZAM FC YATAMBA KURUDI KWA KISHINDO MZUNGUKO WA PILI