Home Azam FC AZAM FC YATAMBA KURUDI KWA KISHINDO MZUNGUKO WA PILI

AZAM FC YATAMBA KURUDI KWA KISHINDO MZUNGUKO WA PILI


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utarejea kwa kishindo kwenye mzunguko wa pili ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Mzunguko wa kwanza Azam FC ilianza kwa kasi ambapo ilicheza jumla ya mechi 7 bila kupoteza na Aristica Cioaba aliweza kuwa kocha bora ndani ya mwezi Septemba na mchezaji wao Prince Dube alikuwa ni mchezaji bora kwa mara ya kwanza.

Iliyumba na kuanza kuambulia matokeo mabovu ambapo ilipopoteza kwa kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Yanga haikuwa na chaguo zaidi ya kumchimbisha Cioaba ambaye alisema kuwa hakujua sababu ya yeye kupigwa chini.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 17 kibindoni ina pointi 32 na ipo chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa watarudi kwa kasi ile ya mwanzo ili kuwa imara.

“Mzunguko wa pili tunarudi kwa kasi kama ile ambayo tulianza nayo kwani tayari mwalimu ameshawajua wachezaji wake na namna ya kuwatumia.

“Imani yetu ni kuwa imara na tutacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa baada ya kucheza mechi tatu za kirafiki za ndani pale timu ilipokuwa Visiwani Zanzibar,” .

SOMA NA HII  KUMBE AZAM FC HAWANA PRESHA NA UBINGWA WA LIGI