Home Uncategorized KOCHA YANGA AMTAJA MLINDA MLANGO ATAKAYEANZA LANGONI

KOCHA YANGA AMTAJA MLINDA MLANGO ATAKAYEANZA LANGONI

KOCHA wa makipa ndani ya Yanga, Peter Manyika amesema kuwa magolikipa wake wote wapo vizuri kwa ajili ya msimu ujao.

Manyika kwa sasa ana makipa watatu ambao ni pamoja na Farouk Shikalo, Ramadhan Kabwili na Klaus Kindoki ambao wote wanapambania kuwa namba moja.

Manyika amesema kuwa :”Kila mmoja anapambana kwa uwezo wake na kwa programu ambayo nimewapa nina imani wote watakuwa vema msimu ujao.

“Nimewaambia kwamba yule atakayefanya vizuri ndiye mwenye nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza msimu ujao,”.

Kwa sasa Yanga ipo kambini Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 23.

SOMA NA HII  RUVU SHOOTING WAMPAPASA BOSI WAO WA ZAMANI, CHUMA APELEKWA HOSPITALI