Home Uncategorized SHIBOUB WA SIMBA AKUBALI KUTUA YANGA, ATAJA MASHARTI

SHIBOUB WA SIMBA AKUBALI KUTUA YANGA, ATAJA MASHARTI

  KIUNGO mchezeshaji wa Simba raia wa Sudan, Sharraf Eldin Shiboub inaelezwa kuwa amepewa ofa na wadhamini wa Yanga, GSM kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo kwenye msimu ujao.

 

Kiungo huyo hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kujiunga na klabu nyingine itakayomuhitaji katika msimu ujao kutokana na mkataba wake wa mwaka mmoja kumalizika ndani ya Simba huku dalili za kuongezewa mkataba zikiyeyuka.

 

Nyota huyo alitua Simba mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Al Hilal ya Sudan ambapo inaelezwa alisaini kwa dau la Sh Mil 100.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Yanga ilimpelekea Shiboub ofa hiyo, lakini wakashindwana katika dau la usajili ambalo amewatajia mabosi hao ambalo ni siri.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kiungo huyo mwenyewe amekubali kujiunga na Yanga kama watakuwa tayari kutoa dau zuri la usajili ambalo yeye amelitaka na mshahara mnono.


Aliongeza kuwa kiungo huyo juzi alirejea nyumbani kwao Sudan huku akiwaacha mabosi wa Yanga wajadiliane na kama wakifikia makubaliano mazuri, basi wamfuate wakiwa na dau ambalo yeye analitaka ili asaini.


“Yanga imeshindwana kidogo na Shiboub katika dau la usajili na kama wangempa lile ambalo analitaka yeye, basi angeshasaini mkataba kabla ya kurejea kwao Sudan.

 

“Shiboub ametaka dau kubwa ambalo mabosi wa Yanga ambao ni GSM wamelishindwa, lakini bado mazungumzo yanaendelea kati ya mchezaji na Yanga.“Ametoa sharti la kumfuata nyumbani kama Yanga watakuwa na kiasi hicho cha fedha ambacho amekitaka ili asaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Mkurugenzi Uwekezaji wa Yanga, Injinia Hersi Said, juzi alisikika akisema: “Tunaendelea na usajili wetu wa siri wa wachezaji wazawa na kimataifa na mara baada ya kukamilika, basi haraka tutamtangaza mchezaji tuliyefikia naye muafaka mzuri na kusaini mkataba.”

SOMA NA HII  HAPA NDIPO AMBAPO WANAPATAKA YANGA MSIMU HUU, MZUNGU ATAJA NAFASI WATAKAYOMALIZA KWENYE LIGI