Home Habari za michezo SIMBA WAMEPANIA AISEE….WAWEKA MIL 250 KWA KIUNGO TP MAZEMBE…DILI ZIMA LIKO HIVI…

SIMBA WAMEPANIA AISEE….WAWEKA MIL 250 KWA KIUNGO TP MAZEMBE…DILI ZIMA LIKO HIVI…

Tetesi za Usajili Simba

Taarifa kutoka DR Congo, zinasema kuwa, Simba imetumia zaidi ya shilingi milioni 250 kwa ajili ya kukamilisha dili la kiungo wa TP Mazembe, Zemanga Soze ambaye dili hilo lipo njiani kukamilika.

Mido huyo ambaye kwa sasa yupo TP Mazembe, alijiunga na timu hiyo akitokea kwa wapinzani wao wakubwa kwenye Ligi Kuu ya DR Congo, AS Vita.

Chanzo kutoka TP Mazembe, kimesema kwamba, uongozi wa Simba umewasilisha ofa ya dola 110,000 za Kimarekani ambazo ni sawa na Sh 255,996,400 za Kitanzania kwa ajili ya kukamilisha usajili wa mchezaji huyo.

“Simba kama ambavyo nilikuambia tayari wapo katika mazungumzo na timu kwa ajli ya kumpata Zemanga Soze, tayari wameshaleta ofa yao ambayo ni Dola za Kimarekani 110,000, kwa pesa ya Kitanzania inafika milioni 250.

“Nafikiria ukiachana na ofa yao kuwa kubwa, lakini kuna uwezekano mkubwa sana wa Simba kukamilisha dili hili kwa kuwa mchezaji mwenyewe anatamani kutua Simba, kama kila kitu kitakuwa sawa basi mwisho wa wiki hii kila kitu kitakamilika,” kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally, alisema: “Kabla ya dirisha la usajili kufungwa tutafanya utambulisho wa vifaa vya maana ambavyo Wanasimba wote watavifurahia.”

SOMA NA HII  HAWA AZAM FC TUTAJUANA HUKO HUKO MBELE YA SAFARI