Home Habari za michezo KISA KUKALISHWA SANA BENCHI….SURE BOY AVUNJA UKIMYA YANGA…”NILIJUA TOKA MWANZO…”

KISA KUKALISHWA SANA BENCHI….SURE BOY AVUNJA UKIMYA YANGA…”NILIJUA TOKA MWANZO…”


Kiungo mchezeshaji wa Yanga, Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ amekiri kukutana na ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi hicho, lakini kamwe hatakubali kukaa benchi na badala yake atapambania nafasi yake.

Staa huyo amekutana na ushindani wa namba wa viungo kutoka kwa Mganda, Khalid Aucho, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Yannick Bangala na Zawadi Mauya.

Hayo yamesemwa na Sure Boy kuwa kabla ya kukubali kusaini Yanga, alifahamu ushindani atakaokwenda kukutana nao kutoka kwa viungo wa timu hiyo.

“Ngumu kwenda katika timu mpya bila ya kukutana na ushindani, hivyo wakati nachukua maamuzi ya kuja kuichezea Yanga nilifahamu kabisa nakwenda kukutana na ushindani wa viungo bora” amesema Sure boy.

Sure Boy alijiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea Azam FC baada ya kuomba mkataba wake uvunjwe. 

SOMA NA HII  LUIS MIQQUISSONE ATOA AHADI NZITO KWA SIMBA, HUKU AKIWAPA MKWARA HUU YANGA