Home Habari za michezo VIGOGO HAWA WA SIMBA WANAPUMUA SASA BAADA YA MSALA HUU

VIGOGO HAWA WA SIMBA WANAPUMUA SASA BAADA YA MSALA HUU

Habari za Simba SC

Presha ilikuwa kubwa sana kwa wazee wangu wale wawili, Salim Abdallah ‘Try Again’ na Murtaza Mangungu ndani ya Simba Sports Club.

Baada ya Simba kupitia kipindi kigumu cha kuangusha pointi katika michezo kadhaa ya ligi na mashindano ya kimataifa basi kelele zikawa nyingi kwamba wazee hao wawili wang’atuke madarakani.

Jambo lililonishangaza ni kwamba walikuwa wanalazimishwa Mangungu na Try Again wajiweke kando lakini ndugu mwekezaji ambaye ana umiliki wa asilimia 49 za hisa za klabu hiyo hakuwa katika shinikizo lolote la kuambiwa naye ang’oke.

Huyu naye kimsingi alipaswa kuwajibishwa kipindi kile cha vuguvugu la kutaka Mangungu na Try Again wajiuzulu kwa vile ndiye ana wajibu wa kuiwezesha Simba kiuchumi hivyo kama kuna mambo hayaendi sawa hasa yanayohusu fedha basi naye anatakiwa kuwajibika.

Lakini ndio hivyo sisi mashabiki wa soka la Bongo huwa ni wazito kumwajibisha tajiri na hata tukibaini amekosea basi tutaangalia wanyonge ni kina nani kisha tunaanza kuwashughulikia.

Hata hivyo, baada ya Simba kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi na kumleta Abdelhak Benchikha na jopo lake, mambo yanaonekana kuiendelea vyema hivi sasa kwa ndani na hata kimataifa tangu kocha huyo alipoanza kazi.

Timu imepoteza mechi moja tu chini ya Benchikha na imeshinda mbili huku ikitoka sare moja na inapiga mpira mwingi na wachezaji baadhi ambao walionekana wamechemsha ni kama wanafufuka upya kutokana na kiwango bora ambacho wamekuwa wakikionyesha.

Na inapofanya vizuri, zile kelele ambazo zilishamiri kutoka kwa wanasimba walio wengi za kutaka Mangungu na Try Again wajiuzulu hazisikiki tena na wote sasa hivi wanatamba na Simba yao huku sifa nyingi zikielekezwa kwa Benchikha.

Kumbe lile shinikizo halikuwa la dhati bwana bali lilitokana na hasira za matokeo yasiyoridhisha, leo timu inashinda wote wako kimya wanajisifia tu na timu yao.

SOMA NA HII  CHAMA NA AZIZ KI WALIVYOMALIZA MICHUANO YA CAF KIBABE...REKODI ZAO NI BALAA...