Home Uncategorized YANGA HESABU ZAO SASA NI KUSEPA NA KOMBE LA LIGI KUU BARA

YANGA HESABU ZAO SASA NI KUSEPA NA KOMBE LA LIGI KUU BARA


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa baada ya kumaliza kazi ya kutwaa taji la Kombe la Mapinduzi nguvu inahamia ndani ya Ligi Kuu Bara.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedrick Kaze inafikisha jumla ya mataji mawili ya Kombe la Mapinduzi kabatini huku mtani wake Simba akiwa na mataji matatu kibindoni.

Kikosi hicho kilitwaa ubingwa huo kwa kuiadhibu Simba kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kazi ni kubwa kwa sasa wanaiwekeza kwenye ligi.

“Tumetwaa taji la Mapinduzi hii ni furaha kubwa kwetu, kazi ya kwanza imekwisha sasa nguvu zetu inahamia kwenye Ligi Kuu Bara, hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti,” amesema. 

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YAZITAKA POINTI TATU ZA MBAO FC LEO