Home Yanga SC DITRAM NCHIMBI ATIMIZA MWAKA MMOJA BILA KUFUNGA

DITRAM NCHIMBI ATIMIZA MWAKA MMOJA BILA KUFUNGA

 


DITRAM Nchimbi,  mshambuliaji wa Yanga, leo Februari 20 ametimiza mwaka mmoja kucheza bila kufunga.


Mara ya mwisho ndani ya Ligi Kuu Bara alifunga mabao mawili Februari 20, Uwanja wa Mkapa kwa pasi za David Molinga.


Kwa sasa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ikiwa imefunga mabao 34 yeye amehusika katika mabao mawili ambayo alitoa pasi za mabao.


Pasi ya kwanza alimpa Michael Sarpong mbele ya Biashara United,  Uwanja wa Karume, Mara na ya pili alitoa mbele ya Kagera Sugar kwa Tuisila Kisinda.

Hivyo leo anatimiza mwaka mmoja bila kufunga ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara. 

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUWA HATAKUWA KWENYE BENCHI...NABI AFUNGUKA NAMNA WATAKAVYOMSULUBISHA MNYAMA...