Home Uncategorized HAWA IHEFU WATOE DARASA KWA WAKONGWE NAMNA YA KUJIJENGA NA KUBORESHA MIUNDOMBINU

HAWA IHEFU WATOE DARASA KWA WAKONGWE NAMNA YA KUJIJENGA NA KUBORESHA MIUNDOMBINU


MIONGONI mwa timu ambazo zinajipanga kwa upande wa miundombinu kila iitwapo leo licha ya kutokuwa na jina kubwa ni pamoja na Ihefu SportsClub.

Timu hii inashiriki Ligi Daraja la Kwanza na imekuwa ikileta ushindani mkubwa katika harakati za kupambania ndoto ya kupanda Ligi Kuu Bara.

Itakumbukwa kuwa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho walipokutana na Azam FC waliwapa tabu kidogo na kuwafanya mabingwa watetezi Azam FC kuponea kwenye tundu la mikwaju ya penalti.

Maskani yake ni Mkoani Mbeya ndani ya Wilaya ya Mbarali inamiliki Hostel pamoja na basi safi kwa ajili ya usafiri na mambo mengine ambayo ni juu yao kwenye matumizi.

Ikiwa ipo Kundi A kibindoni ina pointi 39 imegongana na Dodoma ambayo ipo nafasi ya kwanza ila Ihefu wao wapo nafasi ya pili kwa tofauti ya idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Ni miongoni mwa timu ambazo zinatoa somo kwa timu kongwe Bongo kutambua namna bora ya uwekezaji na mipango sahihi katika kukuza wachezaji na vipaji pia.


Kwa wakati huu Ligi Ikiwa imesimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ni muhimu viongozi wakapata muda wa kutafakari namna ya kubadilisha mambo yawe tofauti na jana.

Ninawapa tano Ihefu hapo mliposhikilia msiache kazeni ili kuzidi kufukuzia mafanikio zaidi na zaidi.

SOMA NA HII  ZAHERA AIZUNGUMZIA MECHI YA SIMBA VS UD SONGO ' MIMI SIJUI' - VIDEO