Home Uncategorized AC MILAN YAFUNGIWA KUSHIRIKI MICHUANO YA ULAYA

AC MILAN YAFUNGIWA KUSHIRIKI MICHUANO YA ULAYA


Klabu ya soka ya AC Milan ya Italy yenye makazi yake katika uwanja wa San Siro itatumikia kifungo cha mwaka mmoja kutokushiriki michuano ya Ulaya inayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) ikiwa ni Klabu Bingwa Ulaya na Europa Ligi.

Klabu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya tano kwenye ligi ya soka Italia, Serie A,  imekumbana na kifungo kutoka kwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo baada ya kuvunja sheria ya ‘Financial Fair Play’ na hivyo haitashiriki michuano ya Europa ya msimu ujao.

Kuna uwezekana mkubwa kuwa kwa sasa nafasi yao ya kushiriki Ligi ya Europa itachukuliwa na Torino, iliyomaliza katika nafasi ya saba kwenye Ligi ya Serie A msimu uliopita. Roma iliyokuwa nafasi ya sita ilishafuzu.

Milan ilifanikiwa kukata rufaa dhidi ya kifungo cha miaka miwili ilichopewa awali na UEFA msimu wa majira ya joto uliopita baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja sheria  hiyo ya ‘Financial Fair Play’

SOMA NA HII  NDEMLA ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA