Home Uncategorized SVEN: TUNA KAZI NGUMU YA KUFANYA KIMATAIFA

SVEN: TUNA KAZI NGUMU YA KUFANYA KIMATAIFA


 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa licha ya kushinda mchezo wa kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa hatua ya awali bado kazi haijaisha lazima wajiweke sawa kwa ajili ya mchezo wa marudio.


Jana, Novemba 29, Simba ilishinda bao 1-0 dhidi ya Plateau United kwenye mchezo wa awali ya Ligi ya Mabingwa nchini Nigeria uliochezwa Uwanja wa New Jos.


Bao la ushindi lilifungwa na nyota Clatous Chama dakika ya 53 kwa pasi ya kiungo mwenzake Luis Miquissone.


Sven amesema:”Wapinzani wetu wana nguvu na walijaribu kiufundi kutafuta goli lakini walishindwa kutokana na uimara wa wachezaji wangu katika hilo ninawapongeza.


 “Matokeo tuliyopta ni mazuri lakini bado hatujamaliza kazi kwa sababu wiki ijayo tuna dakika 90 zingine.” amesema.

Mchezo wa marudio kwa timu hizi unatarajiwa kuchezwa Desemba 5, Uwanja wa Mkapa na Simba inahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote ili isonge mbele hatua ya mtoano.

SOMA NA HII  MASHUJAA WA USWAHILINI; SAMATTA, KIBA, TUWAUNGE MKONO NIA YAO NJEMA YA KUIRUDISHIA JAMII