Home Habari za michezo MSUVA AFUNGUKA MAZITO ALIYOFANYIWA NA WAARABU….ADAI ANAPACHUKIA SANA MOROCCO….”WALINIFUNGIA….”

MSUVA AFUNGUKA MAZITO ALIYOFANYIWA NA WAARABU….ADAI ANAPACHUKIA SANA MOROCCO….”WALINIFUNGIA….”

Aliyekuwa mchezaji wa Wydad Casablanca ya Morocco, Simon Happygod Msuva amesema kwa sasa hataki tena kurudi kucheza soka nchini humo huku akiongeza kuwa hataki kabisa kusikia habari za Wydad.

kauli hiyo ya Msuva inakuja baada ya kuwashtaki Wydad kwa kukiuka masharti ya mkataba wake huku akishinda kesi hiyo FIFA na Wydad kuamriwa wamlipe pesa anazowadai kiasi cha Tsh bilioni 1.6.

“Morocco sitaki hata kupasikia. Kiukweli siwezi na sitaki kurudi tena Morocco. Ni mtu mmoja tu amesababisha mimi nipachukie Morocco ambaye ni Rais wa Wydad Casablanca (Said Naciri). Ilifika steji wakafunga akaunti zangu za benki,” amesema Msuva.

Sasa Msuva yuko huru kujiunga na timu yoyote huku Yanga ikitajwa kumnyemelea staa wao aliyemaliza msimu wake wa mwisho Jangwani akiwa mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 14.

SOMA NA HII  LEO NDIO LEO.....BENCHIKHA AMALIZA KAZI MAPEMA...KOCHA AL AHLY AINGIA UBARIDI WA GHAFLA...

2 COMMENTS

  1. […] Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini, Ramadhani Mbwaduke amesema kuwa Simba SC wanayo nafasi ya kushinda katika mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad AC. […]

  2. […] Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini, Ramadhani Mbwaduke amesema kuwa Simba SC wanayo nafasi ya kushinda katika mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad AC. […]