Home Habari za michezo KISA SIMBA…OKRAH AFUNGUKA ALIVYOZOZANA NA MABOSI ZAKE GHANA…ADAI WALITAKA KUMBANIA ASIJE TZ…

KISA SIMBA…OKRAH AFUNGUKA ALIVYOZOZANA NA MABOSI ZAKE GHANA…ADAI WALITAKA KUMBANIA ASIJE TZ…


Kiungo mshambuliaji mpya wa Simba SC, Augustine Okrah amefanya mahojiano ya kwanza na Msemaji wa Klabu hiyo Ahmed Ally mara baada ya kutua jijini Dar ambapo ameeleza jinsi ilivyokuwa ngumu kuamua kuichezea Simba.

Amesema, alipoletewa ofa na Simba, alivutana na uongozi wake wakaanza kuvutana lakini mwisho wa siku walikubaliana na uamuzi wake wa kuwachagua Wekundu hao wa Msimbazi.

“Haikuwa rahisi, tulivutana sana na uongozi wangu lakini baadaye walikubaliana na chaguo langu la kuja Simba,” alisema Okrah.

Nyota huyo ametua Msimbazi na kupewa mkataba wa miaka miwili ambapo leo Julai 14, 2022 anatarajia kukwea pipa na wachezaji wenzake kuelekea nchini Misri kwa ajili kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

SOMA NA HII  SAKHO, MORRISON WAISHIKA MOROCCO...IBENGE PRESHA JUUU...BANDA AMTISHA MAYELE....