Home Uncategorized YANGA YAANZA KUIVUTIA KASI MTIBWA SUGAR

YANGA YAANZA KUIVUTIA KASI MTIBWA SUGAR


YANGA imeanza kuivutia kasi Mtibwa Sugar kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Jumatano, Julai 22, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Kikosi hicho kitaingia uwanjani kikiwa na kumbukumbu ya kutoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mwadui FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa jana, Julai 18 Uwanja wa Taifa.

Inakutana na Mtibwa Sugar ambayo inapambana kushuka daraja ikiwa imetoka kupokea kichapo cha bao 1-0 mbele ya KMC mchezo uliochezwa Uwanja wa Gairo.

Yanga leo imefanya mazoezi ikiwa ni maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

Mtibwa ikiwa nafasi ya 14 na pointi 41 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 68.

Timu zote zimecheza jumla ya mechi 36 na zimebakiwa na mechi mbili kukamilisha mzunguko wa pili.

SOMA NA HII  SIMBA:ITAKUWA KAZI NGUMU MBELE YA MWADUI FC ILA TUPO TAYARI