Home Azam FC DUBE KUIAGA AZAM JUMATATU

DUBE KUIAGA AZAM JUMATATU


MSHAMBULIAJI wa kikosi cha klabu ya Azam, Prince Dube anatarajiwa kuichezea klabu hiyo mchezo wa mwisho kesho Jumatatu dhidi ya Tanzania Prisons, kabla hajaondoka nchini na kwenda kujiunga na kikosi cha timu ya Tainfra ya Zimbabwe.

Dube ambaye mpaka sasa amehusika kwenye mabao 11 ya Azam kwenye ligi akifunga saba na kuasiti mara nne ameitwa katika kikosi cha Zimbabwe kinachojiandaa na michezo miwili ya kufuzu AFCON dhidi ya Botswana na Zambia.

Azam leo ilitarajiwa kuwa mwenyeji wa Tanzania Prison katika mchezo wa ligi kuu uliopaswa kupigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi, kabla ya ratiba hiyo kupanguliwa kutokana na mchezo wa Namungo.

Azam inaendelea kusalia katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi na pointi zao 36 walizokusanya katika michezo yao 20 waliyocheza mpaka sasa.

Akizungumzia kuitwa kwa Dube, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith, ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Mchezo wetu uliopangwa kufanyika leo dhidi ya Tanzania Prisons umeahirishwa mpaka siku ya Jumatatu, hii ni kutokana na mabadiliko ya mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika kati ya Namungo na de Agosto.

“Kuelekea mchezo huo wa Jumatatu, tunatarajia kuikosa huduma ya kiungo wetu Yahya Zayd ambaye alipata majeraha ya bega katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Mbeya City na atakuwa nje kwa wiki sita.

“Lakini pia baada ya mchezo wetu dhidi ya Prisons mfungaji bora wa kikosi chetu, Prince Dube anatarajiwa kuondoka nchini na kwenda kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe ambayo inajiandaa kwa mechi mbili za kufuzu AFCON dhidi ya Botswana na Zambia,”

SOMA NA HII  AZAM FC HAINA KUPOA...TIZI MWANZO MWISHO