Home Habari za michezo WACHEZAJI SIMBA WAPEWA MASHARTI HAYA…ASIYEWEZA AONDOKE

WACHEZAJI SIMBA WAPEWA MASHARTI HAYA…ASIYEWEZA AONDOKE

WACHEZAJI SIMBA WAPEWA MASHARTI HAYA...ASIYEWEZA AONDOKE

MASTAA wa Simba wamepewa masharti mawili na kocha wa timu hiyo Roberto Oliviera Robertinho na kama watayafuata wataweza kwenda naye sawa.

Kocha huyo raia wa Brazil amesema staa yeyote wa Simba akiwepo uwanjani anatakiwa kujua kwamba ana mambo mawili ya kutimiza moja ni malengo ya timu na la pili kujipa thamani yeye mwenyewe.

Kiufundi alisema anafanya kazi yake kama inavyotakiwa, hivyo wachezaji pia lazima wawe na mtazamo mpana wa kufanya majukumu yao kikamilifu, wakijua soka linatazamwa na watu wengi duniani.

Kundi la kwanza la wachezaji wa Simba limeondoka leo saa tano asubuhi kwenda kwenye mchezo wa kukamilisha ratiba wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca na wachezaji wengine waliopo kwenye timu za taifa wataifuata timu hiyo baada ya kumaliza michezo ya kufuzu AFCON.

“Majukumu yangu ni kuwafundisha mbinu na ufundi ambao wanatakiwa kuutafsiri wawapo uwanjani, kwasababu mchezaji akicheza vizuri ni faida kwake na timu yake kupata matokeo ya ushindi, haya mambo mawili, lazima mchezaji ayafahamu na ayafuate.”

Aliongeza “Kila mmoja ninapompa nafasi ya kucheza anapaswa kuitumia kwa umakini, ili huduma yake iendelee kuifaa timu na yeye mwenyewe afaidike, maana kila mmoja yupo kwa ajili ya Simba.”

Alizungumzia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (Caf) dhidi ya Raja Casablanca, kwamba pamoja na ugumu wa mchezo huo ila anaamini wachezaji wake wanaweza wakafanya vitu vikubwa endapo tu kila mmoja akiutazama mchezo huo kwa jicho la tofauti.

“Ni mechi ngumu wachezaji wapo tayari kwenda kupambana kwa kadri wawezavyo, jambo la msingi wawapo ndani ya uwanja, waonyeshe viwango vyao na kuhakikisha wanaipambania na kulinda brandi ya Simba,” alisema.

Hivi karibuni kocha huyo alisema timu hiyo itakuwa na mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake cha kwanza, huku akiahidi kuwa anataka kuona wachezaji wake wengi ambao wamekuwa hawapati nafasi kwenye michuano hiyo wanacheza na kuonyesha uwezo mkubwa.

Simba imetinga hatua ya robo fainali baada ya kuvuna pointi tisa, ilichapwa bao 1-0 ugenini na Horoya ikashinda marudiano 7-0 Uwanja wa Mkapa, ilishinda ugenini na nyumbani dhidi ya Vipers ya Uganda kwa jumla ya mabao mawili, ilichapwa mabao 3-0 na Raja na inacheza mchezo wa marudiano

SOMA NA HII  KUHUSU BEKI KATILI MCAMEROON KUTUA SIMBA...UKWELI WOTE HUU HAPA...