Home Habari za Yanga KIUNGO WA YANGA ATIKISA SHIRIKISHO…ALIKAA BILA TIMU NUSU MSIMU

KIUNGO WA YANGA ATIKISA SHIRIKISHO…ALIKAA BILA TIMU NUSU MSIMU

Habari za Yanga SC

NI Mudathir Yahya pekee kwenye msitu wa mastaa wa kigeni kwenye mashindano ya kimataifa hatua ya makundi ambapo Simba (Ligi ya Mabingwa) na Yanga (Kombe la Shirikisho Afrika), zote zikiwa zimetinga hatua ya robo fainali aliyeweza kuweka rekodi.

Mudathir amejiunga na Yanga dirisha dogo la usajili akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na waajiri wake wa zamani Azam FC ambao hawakuweza kumuongeza mwingine na kujikuta akikaa nje ya uwanja nusu msimu akifanya mazoezi na KMKM ya Zanzibar.

Wawakilishi wa Tanzania wamebakiza mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba kwenye hatua ya makundi zote zinatoka kwenda kucheza ugenini, Raja Casablanca atakuwa wenyeji wa Simba Aprili 2 huku TP Mazembe akimkamkribisha Yanga Aprili 1.

Simba ambao wanashiriki Ligi ya Mabingwa wamefunga mabao tisa hatua ya makundi wakishinda mechi tatu na kufungwa michezo miwili ambapo wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara nne.

Kwenye mabao tisa ya Simba yote yamefungwa na mastaa wa kigeni ambao ni Clatous Chama raia wa Zambia, aliyefunga manne akiifunga Vipers kwenye ushindi wa bao 1-0 nyumbani na amefunga mabao matatu dhidi ya Horoya wakiibuka na ushindi wa mabao 7-0.

Mabao mengine yamefungwa na Jean Baleke raia wa DR Congo (2) kwenye mchezo dhidi ya Horoya, Henock Inonga raia wa Congo (1) la ushindi kwa Simba ugenini dhidi ya Vipers FC na Sadio Kanoute raia wa Mali ameifungia Simba mabao mawili dhidi ya Horoya.

Kwa upande wa Yanga, mastaa wake watano ndio wamehusika kwenye ufungaji wa mabao huku mmoja kati yao ni mchezaji wa mzawa ambaye amejiunga na timu hiyo dirisha dogo.

Mabao nane ya Yanga wageni wamehusika kwenye mabao saba na Mudathir akihusika kwenye bao moja tu kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe mengine yalifungwa na Keneth Musonda raia wa Zambia na Tuisila Kisinda raia wa Congo.

Huku Fiston Mayele ambaye pia ni raia wa Congo akifunga jumla ya mabao matatu dhidi ya Real Bamako nyumbani na ugenini na dhidi ya US Monastir, bao lingine la Musonda alifunga dhidi ya Real Bamako kwenye ushindi wa mabao 2-0 la pili lilifungwa na Jesus Moloko raia wa Congo.

MWENYEWE AFUNGUKA
Mudathir alipiozungumza na SOKA LA BONGO alisema Yanga inacheza kwa kushirikiana na kila mchezaji ana malengo ya kuona timu inapata matokeo hivyo akipata nafasi ya kufunga ataendelea kufunga na bao alilofunga kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe lina maana kubwa kwake.

“Juhudi binafsi na ushirikiano mzuri baina yetu kama wachezaji ndio siri ya mafanikio lakini kuhusu kufunga bao moja ndio nafasi niliyoipata na endapo nitapata nafasi nyingine nitaendelea kufanya hivyo lengo ni kuona timu inapata matokeo.” alisema Mudathir.

SOMA NA HII  METACHA ATAJWA KUJIWEKA KANDO NDANI YA KIKOSI CHA YANGA