Home Habari za michezo KUHUSU USAJILI MPYA YANGA…NABI AKUNJUA MAKUCHA…MWAKALEBELA AMTUPIA MPIRA…

KUHUSU USAJILI MPYA YANGA…NABI AKUNJUA MAKUCHA…MWAKALEBELA AMTUPIA MPIRA…


KATIKA kuhakikisha anakuwa na kikosi imara atakachokitumia katika michuano ya kimataifa msimu ujao, Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, ametoa masharti ya wachezaji wapya atakaowasajili.

Tayari baadhi ya wachezaji wa kigeni wanatajwa kuwaniwa na Yanga akiwemo Stephan Aziz Ki wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Mkongomani, Kazadi Kasengu.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, amesema kuwa, Kocha Nabi amewasilisha ripoti ya awali ya usajili ambayo imeagiza mchezaji mpya atakayesajiliwa ni lazima awepo katika kikosi cha kwanza katika timu anayoichezea.

Bosi huyo alisema kikubwa kocha hataki mchezaji wa kumpa muda, badala yake anataka wa kuingia moja kwa moja kikosini kama ilivyo kwa Fiston Mayele, Djuma Shaban, Yannick Bangala, Djigui Diarra, Jesus Moloko na Khalid Aucho.

Aliongeza kuwa, msimu ujao malengo yao ni kufanya vizuri katika michuano ya ndani na kimataifa, hivyo katika wale ambao wataondoka, ni wasiokuwa na nafasi.

“Kamati ya Mashindano tayari ina taarifa ya wachezaji wapya wanaohitajika na kocha hadi hivi sasa wakati ligi ikielekea kumalizika. “Kocha ametoa mapendekezo ya wachezaji wa kigeni ambao anawahitaji bila ya kuwataja majina yao na timu zao, anachotaka ni wale ambao wanapata nafasi kikosi cha kwanza katika klabu zao.

“Kocha hataki mchezaji wa kumpa muda, uzuri yeye mwenyewe anafuatilia michuano mbalimbali ya Afrika, hivyo kwake itakuwa nafuu kuwapata wachezaji bora wenye viwango vikubwa na watakaokidhi ubora wa kuleta makombe,” alisema bosi huyo.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alipotafutwa kuzungumzia hilo, alisema kwa kifupi: “Muda wa usajili bado, kila kitu kinachohusiana na usajili kipo kwa kocha Nabi.

SOMA NA HII  BAADA YA USAJILI MZITO WALIOUFANYA ...SINGIDA BIG STARS WAANZA 'KUCHARAZA WATU'....KASEKE ATAKATAKA KAMA 'JUA'....