Home Habari za michezo BAADA YA SIMBA KUTOLEWA CAF….MO KUYAJENGA UPYA NA BENCHIKHA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

BAADA YA SIMBA KUTOLEWA CAF….MO KUYAJENGA UPYA NA BENCHIKHA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Simba leo

RAIS wa heshima na Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji, amesema mwisho wa msimu atakutana na kocha mkuu Abdelhak Benchikha kwaajili ya kufanya tathimini ya kina na kukifanyia maboresho makubwa kikosi hicho.

Simba wameondolewa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, kwa jumla ya mabao 3-0 katika michezo yote miwili nyumbani na ugenini, ikiwa ni mara ya tano katika hatua hiyo.

Mo Dewji amesema ameangalia mechi zote, ameona jinsi gani wachezaji walivyopambana na anaimani na utendaji wa benchi la ufundi na anatarajia kukutana na kocha kwa ajili ya kuangalia mapungufu ya timu yao na kufanya maboresho.

Amesema watafanya maboresho kulingana na mahitaji ya kocha Benchikha, kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo kuleta wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa kuwatoa kusonga mbele katika michuano ya kimataifa.

“Naipenda Simba sana, inapofanya vibaya naumia, tumefanikiwa kucheza robo fainali mara nyingi, tutafanya mabadiliko mwishoni mwa msimu huu kuboresha kikosi chetu kwa kuleta wachezaji wenye uzoefu kwa kuzingatia mapendekezo ya benchi la ufundi,”

Pia amesema baada ya kukamilika kwa msimu anatarajia kukutana na kocha wao kwa ajili ya kufanya tathimini ya timu ikiwemo maboresho ya wachezaji, wataongeza nguvu kwa kuimarisha timu hiyo kutoka hatua ya robo hadi nusu fainali.

Ameongeza kuwa matarajio yake makubwa maboresho yatakayofanyika kwa msimu ujao unaweza kufikia malengo yao, akiamini kuwa hatua ya kufika nusu itakuwa taratibu kama ilivyo kwa hapo awali hakuna mtu ambaye anaamini Simba ingecheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inashuka dimbani leo kusaka nafasi ya kufuzu robo fainali ya Kombe la CRBD Bank Federation dhidi ya Mashujaa FC, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma

SOMA NA HII  KIUNGO MGANDA AWACHANA MUDAHTIR NA BANGALA...AWATOBOLEA SIRI MECHI NA MAZAMBE