Home Habari za michezo KIUNGO MGANDA AWACHANA MUDAHTIR NA BANGALA…AWATOBOLEA SIRI MECHI NA MAZAMBE

KIUNGO MGANDA AWACHANA MUDAHTIR NA BANGALA…AWATOBOLEA SIRI MECHI NA MAZAMBE

KIUNGO MGANDA AWACHANA MUDAHTIR NA BANGALA...AWATOBOLEA SIRI MECHI NA MAZAMBE

Kiungo mkabaji wa Yanga, Mganda, Khalid Aucho amewataka wachezaji wenzake akiwemo Mudathir Yahya na Yannick Bangala kutobweteka watakapokwenda kucheza dhidi ya TP Mazembe ugenini.

Yanga inatarajiwa kurudiana na TP Mazembe kesho Aprili 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa TP Mazembe uliopo katika Mji wa
Lubumbashi nchini DR Congo ukiwa ni mchezo wa mwisho wa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1 yaliyofungwa na Kennedy Musonda, Mudathir Yahya na Tuisila Kisinda.

Licha ya kuripoti kambini, lakini Aucho sambamba na Djuma Shaban na Djigui Diarra hawatakuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi za njano.

Akizungumza nasi, Aucho alisema kwao kila mchezo wanauchukulia kama fainali, hivyo anaamini wachezaji wenzake watapambana kuhakikisha wanafanikisha malengo yao.

Aucho alisema kuwa malengo ya timu ni kumaliza Kundi D wakiwa kileleni na hilo linawezekana kwao, licha ya baadhi ya wachezaji kukosekana, lakini wapo wengine watakaoziba nafasi zao.

Aliongeza kuwa, wachezaji wenzake watatimiza vizuri majukumu yao ya uwanjani yatakayowapa ushindi, licha ya kuwepo ugenini.
“Tunafahamu TP Mazembe watakuwa na sapoti kubwa ya mashabikiuwanjani siku hiyo ya mchezo, lakini hiyo haitufanyi tuhofie.

“Uzuri ni kwamba Yanga ina wachezaji wengi wenye uwezo na uzoefu wa kucheza mashindano makubwa ya kimataifa ugenini, hivyo hiyo haitupi hofu kabisa.

“Kwa pamoja wachezaji tumekubaliana kucheza kitimu kwa kushirikiana ili tufanikishe malengo yetu, hiyo ndio siri kubwa ya mafanikio kwetu Yanga,” alisema Aucho.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA ALINOLEWA NA PELE...WALICHEZA TIMU MOJA...ALIMPASIA PASI YA GOLI