Home Habari za michezo ISHU YA BACCA NA YANGA YAZIDI KUVUMA….APEWA MBINU ZA KUNG’ANG’ANIA JAMBO LAKE…

ISHU YA BACCA NA YANGA YAZIDI KUVUMA….APEWA MBINU ZA KUNG’ANG’ANIA JAMBO LAKE…

Habari za Yanga

BEKI wa kati ya Yanga na timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ bado gumzo kwa wadau wa soka nchini, huku kocha wa timu hiyo, Nasredinne Nabi akipongezwa kumuamini kwenye mechi ngumu na kisha kupewa maujanja ya kuendelea kung’ara kikosini.

Bacca aliyesajiliwa dirisha dogo la msimu uliopita akitokea KMKM, ameonyesha uwezo mkubwa kwenye mechi za kimataifa za Yanga na Stars akipangua ngome ya timu hizo akiingia kikosi cha kwanza, huku Nabi akisifiwa kumbeba hadi kuonwa na kocha wa Stars, Adel Amrouche.

Pongezi hizo zilitolewa na kocha mwenye Leseni ya Diploma A ya Shirikisho la Soka Afrika(CAF), Maka Mwalwisi aliyesisitiza benchi la ufundi la Yanga chini ya Nabi limetimiza jukumu kwa kupandisha viwango vya wachezaji na kuleta maingizo mapya yanayoendana na mahitaji ya timu.

Mwalwisi alisema baada ya Nabi kubaini nyota fulani ni tegemeo hawawezi kuwa kwenye kiwango cha juu wakati wote, alifanya uamuzi makini kwa kuleta mbadala akiwamo Bacca ambaye hajamuangusha.

“Moja ya majukumu ya kocha ni kuhakikisha viwango vya wachezaji vinapanda kila siku na anaingiza maingizo mapya sawa na mahitaji ya timu kwa sababu wachezaji mahiri hawawezi kuwa bora kwa kipindi chote, hivyo unapokosekana ubora kwenye eneo fulani lazima awe na mbadala,”alisema.

Kocha huyo wa zamani wa Mbeya Kwanza na Ihefu, alisema Bacca anapaswa kuwa msikivu kwa makocha na kuwa tayari muda wowote atakapohitajika uwanjani huku akimtaka kutokuwa na majivuno baada ya kuanza kuaminiwa.

“Tabia alizokuwa nazo wakati anaandaliwa zisitoke, asijae majivuno.”

SOMA NA HII  MSAUZI KUPEWA U-CEO SIMBA....KAJULA AANZA KUAGA WACHEZAJI....ISHU NZIMA IKO HIVI...