Home Habari za michezo TETESI ZA USAJILI:KISA BOCCO….MNIGERIA AJIVUTA KIAINA MSIMBAZI….AFICHUA DILI LAKE LILIVYO…

TETESI ZA USAJILI:KISA BOCCO….MNIGERIA AJIVUTA KIAINA MSIMBAZI….AFICHUA DILI LAKE LILIVYO…

Habari za Simba

Kiungo mkabaji wa Rivers United ya Nigeria, Joseph Onoja, anatamani siku moja kucheza pamoja na mshambuliaji wa Simba, John Bocco.

Mnigeria huyo ni kati ya wachezaji waliokuwepo katika mipango ya kusajiliwa na Simba kwa ajili ya msimu ujao anayetajwa kuja kuchukua nafasi ya Ismail Sawadogo.

Kiungo huyo hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu yoyote itakayomuhitaji kutokana na kubakisha miezi sita katika mkataba wake.

Akizungumza nasi, Onoja alisema kuwa anaheshimu ubora wa Bocco katika kufunga mabao, hivyo anatamani kucheza naye katika kikosi cha Simba.

Onoja alisema kuwa amepata taarifa za kuhitajika na Simba kwa ajili ya msimu ujao kutoka kwa meneja wake, kama mazungumzo yakienda vizuri basi ndoto zake zitatimia kwa kucheza pamoja na Bocco.

Alisema kuwa anamfuatilia kwa ukaribu Bocco akiwa anaichezea Simba, uwezo na umahiri mkubwa alionao wa kufunga mabao ndiyo unamvutia.

“Simba ina wachezaji wengi wazuri na bora ambao ningetamani kucheza nao, lakini kubwa zaidi natamani nicheze na Bocco. Ni mshambuliaji ambaye ana uwezo mkubwa wa kufunga ambaye kama nikicheza naye tutakuwa na muunganiko mzuri.

“Nimekuwa nikiifuatilia ligi ya huko Tanzania kwa muda mrefu, hiyo ndio sababu ya kumfahamu vizuri Bocco,” alisema Onoja ambaye aliingia katika kikosi bora cha wiki wa mchezo wa tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi msimu huu.

SOMA NA HII  FT: SIMBA SC 5 - 0 MTIBWA SUGAR ....SAKHO AIBUKA NA STAILI MPYA...AKPAN AKUMBUKWA...