Home Habari za michezo KISASI CHA MIAKA 23 KULIPWA LEO..? YANGA KUINGIA KININJA….MAMELOD WASHTUKA MAPEMA…

KISASI CHA MIAKA 23 KULIPWA LEO..? YANGA KUINGIA KININJA….MAMELOD WASHTUKA MAPEMA…

Habari za Yanga leo

BAADA ya miaka 23, kupita leo Yanga wanakutana kwa mara ya pili dhidi ya Mamelodi Sundowns, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo safari hii wanakutana katika robo fainali.

Awali timu hizo zilikutana katika hatua ya mtoano ilikuwa 2001 katika michezo ya hatua ya awali ya michuano hiyo ambapo katika mchezo wa kwanza Mamelodi Sundowns ilishindikana mabao 3-0 wakati mchezo wa marudiano uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Yanga ililazimishwa sare ya mabao matatu kwa matatu.

Yanga leo wanashuka dimbani katika mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam saa 3:00 usiku.

Yanga wamemaliza katika nafasi ya pili katika Kundi D nyuma ya Al Ahly, wanapania kuwavuruga Mamelodi, Sundowns. Vijana hao wa Rhulani Mokwena wanatamani sana kupata medali ya pili tangu walipoinyanyua mwaka wa 2016 chini ya kocha Pitso Mosimane.

Mamelody Sundowns ilitinga nusu fainali msimu uliopita baada ya kutolewa na Wydad Casablanca, kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mlinda mlango namba moja wa Mamelodi Sundowns, Ronwen Williams atakuwa muhimu kwa Sundowns lakini nyanda huyo anatambua hatari aliyo nayo mshambuliaji wa Yanga, Joseph Guede.

Kurejea kwa nahodha Themba Zwane, alikuwa katika kiwango kizuri kwenye timu ya Taifa ya Afrika Kusini ‘ Bafana Bafana’, kiungo huyo mbunifu atakuwa mmoja wa wachezaji wa kutazamwa katika pambano hili muhimu.

Lakini ni faida kwa kocha Miguel Gamondi ambaye alikuwa akiinoa Mamelodi Sundowns na kushinda taji la ligi mwaka wa 2006, mwalimu huyo anapambana na mpinzani anayemfahamu.

Ingawa huwezi kusema ana ufahamu wa jinsi Mamelodi Sundowns inavyocheza chini ya Rulan Mokwena, anatafuta taji lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa na baada ya kunyakua taji la Ligi ya Soka ya Afrika mwaka jana, anajivunia mafanikio ya hali ya juu.

Katika mchezo watakosa nyota watatu ambao majeraha akiwemo Khalid Aucho, Yao Koussi na Kibwana Shomari ambao wataukosa mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Kuelekea mchezo huo, Kocha Gamondi amesema ni mechi nzuri na kubwa kwa Tanzania, Mamelodi Sundowns ni timu kubwa Afrika, hawakuwa na maandalizi mazuri kwa sababu ya nyota saba kwenye timu za taifa.

“Tupo tayari kwa mchezo huo kutokana na michezo ipo miwili hali hiyo lolote linaweza kutokea, bado nina wachezaji wawili majeraha analazimika kuwa na mbinu mbadala kushinda mchezo huo,” amesema Gamondi.

Ameongeza kuwa hajaona changamoto yoyote ile kwa kocha wa Mamelodi Sundowns, Mokwena kuwafahamu na kuwachambua wachezaji wake katika nafasi na jinsi wanavyocheza ni jambo la kawaida na amejipanga kwa ajili ya kutafuta matokeo mazuri.

Gamondi amesema atawakosa wachezaji watatu ambao ni majeraha akuwemo Aucho, Yao na Shomari na kuwapa majukumu kwa nyota wengine ambao wanaimani ya kufanya vizuri, lakini pia kuna nyota wawili , Djigui Diarra na Aziz Ki wamejiunga na timu asubuhi ya jana (juzi) baada ya kutoka katika majukumu ya timu zao za Taifa .

Mchezaji wa Yanga, Zawadi Mauya amesema wako tayari kwa ajili ya mchezo wao wa leo kuhakikisha wanapambana kutafuta matokeo mazuri ambayo watayapata hapa nyumbani.

“Nusu ya wachezaji walicheza fainali ya msimu uliopita imetusaidia kufikia hatua hii, ninaimani kwa ushirikiano wa wachezaji wote tutafanya vizuri,” amesema Mauya.

Kocha Mokwena amesema amekuja kucheza na timu yenye historia kubwa Tanzania na wanafanya maandalizi mazuri na wako tayari kwa mchezo mgumu dhidi ya Yanga.

Amesema kitu muhimu ni maandalizi mazuri na wanaenda kucheza mchezo wa leo kwa umakini na tahadhari kubwa kwa sababu alifanikiwa kuwaona Yanga katika mechi kubwa za hivi karibuni.

“Niliwaangalia katika mchezo dhidi ya Simba na Azam FC, pia kocha wao amewahi kufundisha Mamelodi Sundowns, haitakuwa mechi tahisi lakini tumefanya maandalizi mazuri na tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Yanga,” amesema Mokwena.

Ameongeza kuwa malengo yake makubwa ni kumaliza mchezo katika mechi hii ya kwanza lakini haitakuwa ngumu kwa sababu ya mpinzani wanayekutana nao.

Amesema mchezo atacheza kwa tahadhari kutokana na ubora wa Yanga, timu ngumu kwa sababu ukiona wachezaji wake ikiwemo safu ya ulinzi ikiongozwa na Ibrahim Bacca na Dickson Job.

“Mbali na safu ya ulinzi lakini kiungo kuna Khali Aucho, Yao Koussi, Joyce Lomalisa, Stephen Aziz Ki na safu ya ushambuliaji kuna Guede, Clement Mzize na Kennedy Musonda najua kila mmoja na uwezo wake, hatuwaogopi bali tunawaheshimu Yanga,” amesema Mokwena.

Kipa wa Mamelodi Sundowns, Denis Onyango amesema aliwahi kusaini Yanga (2010) lakini baadae nilipata ofa na kusajiliwa timu Mamelodi, utakuwa mchezo mzuri kwa sababu kila mmoja amefanya maandalizi mazuri.

“Hakuna timu ndogo kwa sababu wote tunacheza 11, wote tupo level moja. Lakini tupo tayari kwa mchezo wetu kuhakikish tunapata matokeo mazuri dhidi ya Yanga,” amesema Onyango.

SOMA NA HII  CHANONGO AWAONYA MASTAA WENZIE KWENYE ISHU HII