Home Uncategorized SIMBA YAIPOTEZA MAZIMA YANGA NDANI YA DAKIKA 270

SIMBA YAIPOTEZA MAZIMA YANGA NDANI YA DAKIKA 270


KLABU ya Simba imewapoteza nyota wa Klabu ya Yanga kwa kucheka na nyavu kwenye mechi tatu za Ligi Kuu Bara ambazo ni sawa na dakika 270 baada ya ligi kuendelea pale ilipoishia.
Hakukuwa na mechi za ushindani tangu Machi 17 baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona. Serikali iliridhia masuala ya michezo kuendelea tangu Juni Mosi ambapo ligi ilendelea kuanzaia Juni 13.
Yanga imefunga jumla ya mabao manne baada ya kuendelea kwa mechi za ligi na kufungwa mabao matatu, huku Simba ikifunga mabao sita na kufungwa bao moja wakati ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Ruvu Shooting.
Mechi za Yanga zilikuwa namna hii:-Mwadui 0-1Yanga, Juni 13, Uwanja wa Kambarage, mtupiaji wa Yanga alikuwa ni Mapinduzi Balama.Juni 17, JKT Tanzania 1-1 Yanga, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, mtupiaji ali kuwa Patrick Sibomana.Juni 24, Yanga 2-2 Namungo, mtupiaji wa Yanga, David Molinga, Uwanja wa Taifa.
Hizi hapa za Simba:-Juni 14, Simba 1-1, Ruvu Shooting, Uwanja wa Taifa, mtupiaji Shiza Kichuya.Juni 20, Simba 3-0 Mwadui FC, watupiaji ni John Bocco, Hassan Dilunga na Samson Augustino alijifunga.Juni 24, Mbeya City 0-2 Simba, mtupiaji alikuwa ni John Bocco.
Bocco ametupia mabao matatu akiwafunika watupiaji wote wa Yanga kwenye mechi tatu za hivi karibuni huku Yanga mtupiaji wao mwenye mabao mengi ni David Molinga akiwa ametupia mabao mawili.
SOMA NA HII  CIOABA WA AZAM FC KUIVAA MBEYA CITY BILA NYOTA WAKE MMOJA