Home Uncategorized PAMOJA NA KUZOMEWA JUZI …MBELGIJI WA YANGA EMESEMA HAYA KUHUYU YIKPE..!!

PAMOJA NA KUZOMEWA JUZI …MBELGIJI WA YANGA EMESEMA HAYA KUHUYU YIKPE..!!

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbelgiji Luc Eymael amejitokeza kifua mbele na kuweka bayana kwamba straika wake Muivory Coast, Yikpe Gislein Gnamien ataendelea kupata nafasi ya kucheza katika kikosi chake.

Eymael amesema tatizo kubwa la straika huyo katika mechi ni kushindwa kukifanya kile anachokifanya mazoezini kiasi cha mshabiki kumuona hafai.

Hivi karibuni mashabiki wa Yanga walikuja juu kutokana na kushuhudia kiwango kidogo cha Yikpe ambaye alisajiliwa katika dirisha dogo msimu huu.

Eymael ameliambia Spoti Xtra, kuwa ni ngumu kwa kile anachokionyesha Yikpe mazoezini kumuacha kutomjumuisha katika mechi na mara nyingi amekuwa akimjenga kwa kumpa ujasiri wa kupambana.

 “Ninasema kila siku kuhusiana na suala la Yikpe, hakuna kocha duniani ambaye anaweza kumchagua mchezaji asiyejituma, kinachotokea kwake anafanya vizuri sana mazoezini.

 “Lakini bahati mbaya anashindwa kufanya vilevile akiwa katika mechi, nimejaribu mara nyingi kumpa ujasiri kwa kumpa nafasi ya kucheza, najua mashabiki wanaanza kuchoka juu ya anachokifanya.

 “Siyo yeye tu, hata Molinga (David) pia nimekuwa nikimpa moyo wa kupambana kwenye kila mechi, nimempa nafasi nyingi na nimekuwa nikimrekebisha mara kadhaa.

 “Mashabiki wanatakiwa kuelewa kwamba siku ya mechi ni kama mtihani, wachezaji wanatakiwa kupafomu kwa sababu tayari nakuwa nawapa kila kitu na siyo kazi yangu kuingia uwanjani kwenda kufunga au kurekebisha kile wanachokikosea,” alisema Eymael.

SOMA NA HII  MESSI ADAI KWAMBA YEYE NI MCHEZAJI HURU ANAWEZA KUSEPA, ISHU MPAKA FIFA