Home Simba SC SIMBA: TUNATAKIWA KUSHINDA MBELE YA YANGA

SIMBA: TUNATAKIWA KUSHINDA MBELE YA YANGA


KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Yanga, kesho Mei 8, 2021 uongozi wa Simba umeweka wazi kwamba unatakiwa kushinda mchezo huo ili kuongeza nafasi ya kushinda taji la ligi.

Simba ni mabingwa watetezi wa ligi kesho wanakutana na Yanga kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Walipokutana mzunguko wa kwanza Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba na watupiaji kwa Yanga alikuwa ni Michael Sarpong na kwa Simba alikuwa ni Joash Onyango ilikuwa ni Novemba 7,2020.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wana kazi moja ya kufanya kesho kusaka ushindi ili kuongeza nafasi ya kuweza kutetea taji hilo.

“Utakuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani ila lazima tushinde ili tuweze kuongeza nafasi ya kutetea taji letu la ligi.

“Mbali na kucheza pia ni muhimu tufanye kazi ya umiliki wa mpira kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwenye mechi zetu ambazo zimepita ili kuwapa burudani mashabiki hivyo wajitokeze kutupa sapoti hatutawaangusha,”.

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 25 ina pointi 61, Yanga ipo nafasi ya pili ina pointi 57 baada ya kucheza mechi 27.

SOMA NA HII  KUMBE FEI TOTO KAMA NTOBAZONKIZA TU...HAJAACHA KITU YANGA SC AISEE..KABEBA KILA KITU...