Home Habari za michezo PAMOJA NA KUTOA KAFARA YA NG’OMBE …MISRI WACHEZESHWA ‘NDOMBOLO’ NA CONGO…

PAMOJA NA KUTOA KAFARA YA NG’OMBE …MISRI WACHEZESHWA ‘NDOMBOLO’ NA CONGO…

Habari za Michezo

CHAMA cha Soka cha Misri kimefichua kwamba kimechinja ng’ombe kama kafara kwa ajili ya timu yake kufanya vizuri kwenye fainali za Afcon 2023 zinazoendelea huko Ivory Coast.

Msemaji wa chama hicho, Mohamed Morad alisema juzi Ijumaa kwamba ng’ombe amechinjwa na nyama yake imegawawia kwa watu wenye uhitaji huko Cairo ili kuleta bahati kwenye timu hiyo.

Misri bado haijashinda mchezo wowote kwenye fainali za Afcon 2023 na jana Jumapili ilishuka dimbani kukipiga na DR Congo katika mchezo wa hatua ya 16 bora huko San Pedro. Timu hiyo ilitoka mji wa Abidjan hadi San Pedro kwa ajili ya mchezo huo ambao hata hivyo walifungwa kwa penalti

Kambi ya timu ya taifa ya Misri imekumbwa na majeruhi wengi. Imempoteza supastaa wake, Mohamed Salah kwa maumivu ya misuli na kipa Mohamed El Shenawy, aliyeumia bega katika mchezo wao wa tatu.

Emam Ashour Jumatano aliwahishwa hospitali baada ya kuumia kichwani mazoezini, lakini sasa amerejea na kujiunga na kikosi hicho kwa ajili ya mikikimikiki hiyo ya hatua ya mtoano.

Wachezaji wa Misri waliripotiwa kutoa kafara ya mnyama mazoezini kwao kabla ya kushinda ubingwa wa Afcon 2008 katika fainali zilizofanyika Ghana.

Misri 🇪🇬 1-1 🇨🇩 DR Congo (P 7-8 )
⚽ Mostafa Mohamed 45’
⚽ Meschack Elia 37’

MATUTA

MISRI ✅❌✅✅✅✅✅✅❌

DRC  ✅❌✅✅✅✅✅✅✅

DR Congo itachuana na Guinea katika hatua ya robo fainali.

SOMA NA HII  BAADA YA MPOLE KUISUSIA GEITA...NTIBAZONKIZA NAYE AKIWASHA..ASUSA KUJIUNGA NA TIMU...