Home Habari za michezo HII HAPA RATIBA YA MECHI ZA SIMBA KWA MWEZI HUU WA NNE…MECHI...

HII HAPA RATIBA YA MECHI ZA SIMBA KWA MWEZI HUU WA NNE…MECHI NA YANGA MHHH….

Habari za Simba SC

Baada ya mchezo dhidi ya Raja Casablanca uliopigwa huko Morocco usiku wa kuamkia juzi, kikosi cha Simba kimeondoka Morocco kurejea Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata.

Simba inakabiliwa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa April 07 katika uwanja wa Uhuru.

Siku tatu baadae Simba itasafiri Mbarali Mbeya kwa ajili ya mchezo mwingine wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa April 10.

Utafuata mchezo wa dabi dhidi ya Yanga ambao utapigwa April 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika mwezi huu pia mechi mbili za robo fainali ligi ya mabingwa zitapigwa. Droo ya hatua ya robo fainali itafanyika Jumatano, April 05 huko Cairo, Misri

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE