Home Habari za michezo KISA TUZO ZA KINA CHAMA….SIMBA WAVIMBA NA CAF…

KISA TUZO ZA KINA CHAMA….SIMBA WAVIMBA NA CAF…

Habari za Simba SC

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa tuzo ambazo wamekomba wachezaji wake kwenye mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika, (CAF) kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kumewaongezea hali ya kujiamini.

Chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira raia wa Brazil imetinga hatua ya robo fainali huku ikitunguliwa nje ndani na Raja Casabalanca.

Ni Clatous Chama ana tuzo mbili kabatini ikiwa ni ile ya mchezaji bora mechi ya nne pia ana tuzo ya bao bora alilofunga wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 7-0 Horoya ambapo kwenye mchezo huo alifunga hat trick.

Nyota huyo alitajwa kwenye kikosi bora mchezo wanne pamoja na beki Shomari Kapombe kwenye mchezo wa tano alipenye pia kikosi bora akiungana na Jean Baleke,Sadio Kanoute na Kapombe.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa tuzo hizo zinaonyesha ukomavu wa wachezaji wa Simba pamoja na jitihada wanazofanya.

“Kupata tuzo kwa wachezaji wetu na kuwa kwenye kikosi bora hii ni fahari kwetu na inaongeza thamani ya wachezaji pamoja na ukubwa wa timu, pongezi wanastahili na hili linaongeza hali ya kujiamini kwa mechi zetu zote za mashindano ambazo tunacheza.

“Katika hatua ambayo tunakwenda ya robo fainali inaonyesha kuwa ugumu unazidi kuongezeka huku wachezaji wakizidi kuimarika, tunaamini tutafanya vizuri kwenye haya mashindano makubwa kwa kuwa tuna wachezaji imara,” amesema Ally.

SOMA NA HII  HII HAPA RATIBA YA MECHI ZA SIMBA KWA MWEZI HUU WA NNE...MECHI NA YANGA MHHH....