Home Habari za Yanga YANGA SC 1-0 TP MAZEMBE…WANANCHI WAKAA KILELENI…MAZEMBE WAPIGWA CHA UCHUNGU

YANGA SC 1-0 TP MAZEMBE…WANANCHI WAKAA KILELENI…MAZEMBE WAPIGWA CHA UCHUNGU

Habari za Yanga

Wawakilishi wa Tanzania Katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Timu ya Yanga imehitimisha michezo yake ya hatua ya Makundi kwa kushusha dozi katika Uwanja wa Stade Mazembe kwa kuwaadhibu wenyeji TP Mazembe bao 1-0.

Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na Farid Musa alieingia kutokea benchi akichukua nafasi ya Kiungo Mudathir Yahaya Abbas.

Ushindi huo unawapeleka Yanga mpaka kileleni mwa msimamo wa Kundi D, huku wakisubiri mchezo kati ya US Monastir dhidi ya Real Bamako.

Msimamo wa kundi D ulivyo mpk hivi sasa

Yanga Michezo -6 alama 13
Us Monastir Michezo -5 alama 10
Real Bamako Michezo-5 alama 5
Tp Mazembe Michezo-6 alama 3

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa kwa Mkapa Yanga walishinda mabao 3-1.

SOMA NA HII  AHMED ALLY ATANGAZA USHINDI DHIDI YA YANGA....... MVUA YAHUSISHWA