Home Habari za michezo AHMED ALLY ATANGAZA USHINDI DHIDI YA YANGA……. MVUA YAHUSISHWA

AHMED ALLY ATANGAZA USHINDI DHIDI YA YANGA……. MVUA YAHUSISHWA

Habari za Simba SC

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema kitendo cha mvua kunyesha kuelekea kwenye mchezo wao wa dabi, ni ishara nzuri ya ushindi kwao.

Ahmed amefunguka hayo mapema hii leo Novemba Mosi, 2023 alipokuwa kwenye mkutano wa kuwatangaza wadhamini wao wapya Kampuni ya Serengeti Breweries.

“Mvua ni ishara nzuri kwa Simba. Tukiwa katika wiki hii yenye thamani kubwa ya Kariakoo Derby tumewaletea tukio lingine kubwa la kihistoria kati ya Simba na Serengeti,” alisema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  MAKUNDI SIMBA NA YANGA KUJULIKANA OKT 7