Home Habari za michezo AZIZ KI AWAPA KITETE SIMBA KUELEKEA DABI YA KARAKOO

AZIZ KI AWAPA KITETE SIMBA KUELEKEA DABI YA KARAKOO

Habari za Yanga

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga ambaye yupo kwenye kiwango bora hivi sasa, Stephane Aziz Ki, amesema amejiandaa kucheza kwa kupaniwa katika Kariakoo Dabi, huku akibainisha kwamba hiyo itawapa nafasi nyota wengine kufunga mabao akiwemo Mkongomani, Maxi Nzengeli.

Dabi hiyo inatarajiwa kuzikutanisha Simba dhidi ya Yanga, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Spoti Xtra, Aziz Ki alisema katika kila mchezo wa Ligi Kuu Bara, anakutana na upinzani mkubwa kutokana na mabeki kucheza kwa kumpania ili asifunge.

Aziz Ki alisema anafurahia kupaniwa huko, ambako kunatoa nafasi kwa wachezaji wengine kufunga mabao.

“Ubora wa wachezaji uliokuwepo hivi sasa kikosini kwetu, kila mchezaji anafunga na hatumtegemei mchezaji mmoja pekee kama ilivyokuwa msimu uliopita.

“Hivi sasa kama ukinipania mimi kunikaba ili nisifunge, basi atakuwepo mchezaji mwingine atakayefunga kama siyo Maxi, basi atakufunga Pacome (Zouzoua), Mzize (Clement) au Musonda (Kennedy).

“Kuelekea dabi hatuna hofu ya mchezo huo, lakini tunawaheshimu wapinzani wetu Simba ambao nao wamefanya usajili mzuri utakaotupa ushindani katika mechi hii,” alisema Aziz Ki

SOMA NA HII  KWA YANGA HII WAPINZANI TUMBO JOTO, ALLY KAMWE ATAMBA