Home Habari za michezo KUELEKEA DABI YA KARIAKOO SIMBA WALAMBA DILI HILI LA KIBABE

KUELEKEA DABI YA KARIAKOO SIMBA WALAMBA DILI HILI LA KIBABE

Tetesi za Usajili Simba

Katika kuelekea mchezo wao wa Dabi dhidi ya Yanga SC, Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wameingia mkataba wa Bil. 1.5 na Kampuni ya Serengeti Breweries kupitia bia yao ya Pilsner Lager.

Simba wametangaza udhamini huo hii leo Novemba Mosi, 2023 wakati dabi yao inakwenda kupigwa Jumapili Novemba 5, 2023.

“Tunajivunia kuziunganisha taasisi mbili kubwa za SBL na Simba kwa mkataba wa udhamini wa miaka mitatu. Kupitia udhamini huu utaifanya bia yetu ya Pilsner Lager kuwa mdhamini wa Simba.”

“Udhamini huu utakuwa na thamani ya Tsh. 1.5 bilioni. Kwa udhamini huu tunaamini utasaidia kukuza michezo nchini kwetu. Simama Imara, Songa Mbele Kama Simba,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti ​Breweries Limited, Obinna Anyalebechi.

SOMA NA HII  AHMED ALLY : KWA HALI HII INABIDI TUVUKE MAKUNDI KWA NAMNA YEYOTE