Home news BAADA YA KUANZA KUWA STAR UPYA ….TIMU YA DARAJA LA KWANZA YAMUWEKEA...

BAADA YA KUANZA KUWA STAR UPYA ….TIMU YA DARAJA LA KWANZA YAMUWEKEA ULINZI AMISSI TAMBWE


MSHAMBULIAJI wa DTB FC, Amissi Tambwe amewekewa ulinzi maalumu wakati timu hiyo itakapokutana na JKT Tanzania kwenye Ligi ya Championship.

Kocha Mkuu wa timu ya JKT Tanzania, Mohamed Abdallah ‘Bares’ alisema kuwa wanatambua ubora wa mchezaji huyo ila wao kama timu wamejipanga vyema kuhakikisha anashindwa kuonyesha makali yake.

“Nina wachezaji mwenye uzoefu na isitoshe wengi wanamjua Tambwe vizuri kwa sababu wameshacheza nae kwenye Ligi Kuu hivyo sio mgeni kwetu, kikubwa mchezo utakuwa mgumu ila tumejipanga kuibuka na ushindi kwani hayo ndio malengo yetu,” alisema.

Kwa upande wa katibu Mkuu wa DTB, Muhibu Kanu alisema hawajakosea kumpa kitambaa cha unahodha kwani wanajua ni mchezaji kiongozi awapo Uwanjani, huku akisisitiza kuwa huu ni mwanzo tu kwake kwani ataendelea kufunga zaidi msimu huu.

“Wengi walishangaa kumuona mchezaji kama yeye anacheza Ligi ya Championship wakidhani yale makali yake aliyokuwa nayo Ligi Kuu yameisha lakini ukiangalia mpaka sasa watu wanamuongelea zaidi kutokana na mambo makubwa anayofanya,” alisema.

Tambwe ameendelea kuisaidia timu yake kuendeleza wimbi la ushindi baada ya DTB kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya African Sports ‘Wanakimanumanu’, huku akifanikiwa kufunga bao moja na lingine likifungwa na mchezaji wa zamani wa Simba Nicholas Gyan.

kwa sasa nyota huyo amekuwa tishio kwenye Ligi hiyo baada ya kucheza michezo mitatu na kufunga jumla ya mabao sita.

Timu hizo zinakutana Oktoba 23, kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo, huku JKT ikihitaji matokeo ya ushindi baada ya mchezo wa mwisho kulazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3, na Transit Camp.

SOMA NA HII  MORRISON APEWA KAZI MAALUMU BENIN...WAANZA TIZI LA KIBABE...YANGA vs KMC..NI MECHI YA HELA AISEE...