Home Yanga SC BAADA YA KUITEMA YANGA…WAZIRI JR AFUNGUKA A-Z MAISHA YAKE JANGWANI..AWATAJA VIONGOZI

BAADA YA KUITEMA YANGA…WAZIRI JR AFUNGUKA A-Z MAISHA YAKE JANGWANI..AWATAJA VIONGOZI


Nichukue fursa hii kuwashukuru sana wana Yanga kuanzia makocha, wachezaji, viongozi na mashabiki kwa kuniamini na kuwa mmoja wao

Haikuwa safari rahisi licha ya kuwa fupi mno

Nilifika Yanga SC nikiwa na malengo makubwa lakini haikwenda kama nilivyotarajia labda kwa sababu zangu binafsi au vinginevyo

Ni kawaida yetu sisi wanasoka kukutana na changamoto kama hizi.

Nimechukua maumuzi mgumu sana kwangu lakini yote ni kwa maslahi mapana ya ufanisi wangu

Nimeona nihamishie jitihada zangu sehemu nyingine

Yamkini sikufikia malengo ya klabu na kutokuwapa mashabiki ile furaha waliyotarajia kutoka kwangu lakini niwatoe shaka kuwa haikuwa dhamira yangu kuwaangusha

Niwatakie kila la kheri kwenye safari yenu kuelekea msimu ujao. Tuendelee kuombeana labda ipo siku tutakuwa pamoja tena kama sio, basi nitaendelea kuuenzi upendo na imani mliyoijenga kwangu

Najivunia kuvaa nembo ya Klabu Kubwa hapa nchini. Asante (mungu kwanza) @wazir_junior_10

SOMA NA HII  YANGA KUSHUSHA 'MASHINE YA KUFUNGA MAGOLI' KUTOKA WYDAD CASABLANCA