Home Simba SC PAPE SAKHO AANZA KWA KASI YA 5G SIMBA …APIGA GOLI LA KIULAYA...

PAPE SAKHO AANZA KWA KASI YA 5G SIMBA …APIGA GOLI LA KIULAYA ULAYA MECHI IKIISHA KWA SARE


Kikosi cha Simba leo kimecheza mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya AS FAR Rabat ya nchini humo na kumaliza kwa sare ya mabao 2-2.

Simba ilipanga kucheza mechi tatu za majaribio katika kambi yao na tayari ya kwanza imemalizika kwa sare huku winga mpya Pape Ousmane Sakho akifungua kibubu cha mabao kwa Wekundu wa Msimbazi.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Simba kuwa nyuma kwa mabao mawili na baada ya kurudi kipindi cha pili Hassan Dilunga alitupia bao moja na Sakho kumalizia la pili.

Rabat inanolewa na aliyekuwa kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck ambaye aliondoka na nafasi yake kuchukua Didier Gomes.

SOMA NA HII  ISHU YA USAJILI WA ADEBAYOR SIMBA IKO HIVI...KUMBE WAMEPIGWA DANADANA..AHMED ALL AFUNGUKA...