Home Uncategorized KOCHA : KUIZUIA SIMBA KWA SASA KAZI IPO

KOCHA : KUIZUIA SIMBA KWA SASA KAZI IPO

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa inahitaji umakini mkubwa kwa Yanga kuizuia Simba kutwaa ubingwa kutokana na kasi waliyonayo kwa sasa.
Thiery amesema kuwa kikosi cha Simba kimekuwa imara muda mrefu na kinaonyesha dalili za kuuhitaji ubingwa kwa hali jambo linaoongeza ugumu kuzuiwa.
“Ukiitazama kasi ya Simba na namna ambavyo wanaonyesha kasi kwenye kutafuta matokeo bado naona kuna ugumu kwa wapinzani wao ikiwa ni pamoja na Yanga kuizuia kufikia malengo yao hivyo inahitaji kazi ya ziada kuifunga.
“Yanga ni timu imara lakini kinachowatufautisha kwa sasa ni idadi ya pointi pamoja na mechi, naona njia nyepesi kwa Yanga kuizuia Simba ni kushinda mehi zote ikiwa ni pamoja na ile itakayowakutanisha,” amesema Thiery.
SOMA NA HII  KESHO YANGA V AZAM NI BALAA, DATA NI NOMA