Home Habari za michezo SIMBA, YANGA MMBO YAMESHAANZA TENA HUKO WPL

SIMBA, YANGA MMBO YAMESHAANZA TENA HUKO WPL

Habari za michezo

Kumekucha Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), wakati mechi za Ngao ya Jamii zikipigwa leo, huku vigogo Simba Queens, Yanga Princess, JKT Queens na Fountain Gate Princess zikisaka taji hilo linaloshindaniwa kwa mara ya kwanza kwenye ligi hiyo.

Simba na Yanga zenyewe zinavaana leo jioni zitashuka kwenye Uwanja wa Azam Complex katika ufunguzi wa ligi hiyo huku kila timu ikiahidi kupambana ili ivuke na kwenda fainali itakayopigwa Desemba 12.

Mechi hiyo ya Kariakoo Dabi itapigwa saa 12 jioni baada ya ile ya JKT na Fountain Gate Princess itakayochezwa saa 9 alasiri na washindi wa kila mechi ndio watakaocheza fainali hiyo Desemba 12 na kupatikana bingwa wa kwanza nchini.

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Vivian Corazone amesema wanajua umuhimu wa mchezo huo wa mtoano ambao ndio mara ya kwanza kuanzishwa kwa wanawake, hivyo watapambana.

Alisema Yanga Queens ni timu kubwa na kila timu zinatamani kufanya vizuri na wao kama wachezaji watafuata maelekezo ya kocha wao kuhusu nini cha kufanya ili wapate matokeo na kuvuka hatua inayofuata.

“Tunajua ugumu wa mechi na ni muhimu pia kwetu kuandika historia nyingine.”

SOMA NA HII  NABI AAMUA KUSEPA YANGA...CHANZO HIKI HAPA...KAZE ATAJWA...UONGOZI WABARIKI.....