Home Azam FC KWA HAYA YANAYOENDELEA AZAM FC MNAPIGA HESABU VEMA LAKINI?

KWA HAYA YANAYOENDELEA AZAM FC MNAPIGA HESABU VEMA LAKINI?

Habari za Azam

Ukichungulia msimamo wa Ligi Kuu kwa sasa pale kileleni utawakuta Matajiri wa Dar es Salaam, Azam FC wakiwa wamepoa na alama zao 25, baada ya mechi 12, za Ligi Kuu huku uwanjani wakitandaza soka safi.

Unaweza kusema wameamka na sasa wanautaka ubingwa wa ligi ambao wamewahi kuuonja mara moja tu walipobeba kombe msimu wa 2013/2014 bila kupoteza mechi yeyote huku kikosi chao kikiwa kimejaa mastaa watupu.

Kwa sasa Azam inaongoza karibu kwenye kila kitu chanya katika ligi msimu huu kasoro pasi za mwisho za mabao (asisti) anazoongoza Kouassi Attohoula Yao wa Yanga mwenye tano akifuatiwa na Kipre Junior na Feisal Salum ‘Feitoto’ wa Azam walio na nne kila mmoja sambaba na kwenye ‘Cleansheet’ anakoongoza John Noble wa Tabora United akiwa nazo nne.

Wakali hao wa mitaa ya Chamazi, ukitoa kuongoza ligi mbele ya Yanga na Simba zinazofuata, pia ndio timu iliyofunga mabao mengi hadi sasa ikiwa imecheka na nyavu mara 29, ikifuatiwa na Yanga iliyofunga 26 kwenye mechi zake tisa ilizocheza huku Simba ikifuata kwa kufunga 18, katika mechi nane ilizocheza hadi sasa.

Azam pia inaongoza katika ufungaji bora ambapo kiungo Fei Toto ana mabao saba sawa na Jean Baleke wa Simba na Stephane Aziz Ki na Maxi Mpia Nzengeli wote wa Yanga.

Kichapo ilicho kipata mara mbili mfululizo mwezo Oktobas kutoka kwa Yanga (3-2), na Namungo (3-1), ni kama kiliitia hasira timu hiyo kwani baada ya hapo imeshinda mechi zote nne zilizofuata tena kwa mabao yasiyopungua matatu katika kila mechi huku ikifunga jumla ya mabao 16 katika michezo hiyo minne.

Ilianza kwa kuifunga Mashujaa 3-0, ikafuata Ihefu 3-1 zote ikiwa ugenini kabla ya kurejea Dar ilipotembeza dozi ya mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na juzi ikaisulubu KMC mabao 5-0.

WASIKIE WENYEWE

Kocha wa Azam, Msenegali Youssouph Dabo alisema ni muendelezo wa malengo yao msimu huu ambayo tangu amechukua timu ameweka mikakati ya kurejesha soka nidhamu, soka safi na ushindani kikosini hapo.

“Maendeleo ya kile tulichopanga kufanya yako vizuri. Nafurahi kuona kila siku tunaimarika ni jambo zuri na ndio lengo letu kuwa bora kwenye kila eneo kisha kumaliza msimu tukiwa katika nafasi nzuri,” alisema Dabo ambaye ni msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu.

Nyota kinara wa timu hiyo, Fei Toto aliyetua Azam msimu huu akitokea Yanga alisema siri kubwa ya timu yao kucheza kwa ubora ni ushirikiano na kujituma kwa kila mmoja.

“uko vizuri, nadhani kila mtu anatimiza vyema majukumu yake pia juhudi za kila mmoja wetu na ushirikiano.”

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI