Home Habari za michezo UNAAMBIWA HII NDIO TIMU BORA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI

UNAAMBIWA HII NDIO TIMU BORA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI

Habari za Yanga

Yanga kwa sasa inakikosi bora zaidi kwenye ukanda wetu wa Africa Mashariki na kati, kinachovutia zaidi Kocha Gamondi amekutana na kikosi bora sana, Wachezaji ambao Wameingia moja kwa moja kwenye Falsafa zake.

Alichofanikiwa Gamondi kumfanya kila mchezaji kucheza kwenye ubora wake, Aziz Ki, Pacome na Maxi bila kumsahau Khalid Aucho, kila mmoja anacheza kwa uhuru mkubwa bila kuhofia nini kitatokea endapo nitapoteza mpira. Staili hii ya Uchezaji inaitwa “RELATIONISM ” ama kwa Lugha nyepesi ni Jogo Bonito’ “The Beautiful Game “.

Aina hii ya mpira ni maarufu sana America ya kusini kwa sasa inafundishwa timu ya taifa ya Argentina chini ya Lionel Scaloni, Fluminense na timu ya taifa Brazil Fernando Denis na Gremio chini ya Renato Gaucho. Hii ni staili ambayo mchezaji anakua huru kucheza kama yupo kwenye mazoezi tena kwa furaha “Free Stay Style”.

Maxi Nzengeli, Aziz Ki na Pacome wanavyobadilishana nafasi na jinsi wanavyoachiana pasi bila kujali wapo eneo gani ni kitu kizuri kukiona, kumbuka Wamefanya haya yote mbele ya Simba na si Kagera Sugar ama Geita.

Yanga kwa kile ambacho Wamekifanya jana Uwanja wa Benjamin Mkapa itahitaji timu spesho kuifunga timu ya Yanga, kwa kifupi hii ndiyo timu bora kwa sasa kwenye ukanda wetu huu wa Africa Mashariki na Kati, hawakufika hapa kwa bahati mbaya Wameijenga timu yao taratibu mpaka kufikia hapa.

Simba waliwahi kua kwenye hii nafasi ambayo Yanga wapo kwa sasa misimi mitatu ya nyuma, Simba ilikua ikishinda huku ikicheza soka safi lilikua likiitwa PIRA BIRIANI ila Walishindwa kukaa kileleni kwa muda mrefu, Walitengeneza ubora ambao walishindwa kuuendeleza na Yanga Wamefanikiwa kufika kwenye huo ubora.

Kwenye mpira hakuna njia ya mkato kupata mafanikio, uwekezaji ndiyo msingi wa kila kitu na si kuwekeza ila kuwekeza kwenye Wachezaji wenye tija sambamba na benchi bora la ufundi, Yanga imeset standard ya ubora Tanzania hakuna namna ili uwe bingwa ni lazima ufikie ubora wa Yanga na kuupita.

SOMA NA HII  YANGA WAFUNGUKA UWEPO WA GAEL BIGIRIMANA KAMBINI