Home Habari za michezo MAXI, AZIZ KI WAIPONZA SIMBA, MILIONI 300 ZIMEPITA HIVI

MAXI, AZIZ KI WAIPONZA SIMBA, MILIONI 300 ZIMEPITA HIVI

Habari za Yanga SC

Mastaa wa Simba juzi walipoteza Sh300Milioni mkononi baada ya kupoteza mechi dhidi ya Yanga.

Viongozi walikaa na wachezaji Jumamosi jioni kwenye kambi yao Jijini Dar es Salaam na kuwaahidi fungu hilo na wakalitoa taslimu mbele yao.

Iko hivi;Mfadhili wa Simba, Mohammed Dewji kwenye kikao hicho alimuita mbele nahodha John Bocco na kumuonyesha fedha hizo na akazihakiki kwamba ziko Mil 300 kisha akawaambia wenzie; “Kazi kwetu, mzigo uko kamili.”

Mwanaspoti linajua kwamba msaidizi maalum wa Mo, alipewa furushi hilo kwenye begi na akaingia nalo mpaka vyumbani ili kuwapa mzuka wachezaji kushinda mechi hiyo muhimu. Na baada ya kumalizika kwa mchezo huo aliweka mzigo wake begani na kuondoka zake huku wachezaji wakishindwa kuamini macho yao.

Kwa wachezaji 15 waliovaa kwenye mechi hiyo kila mmoja alikuwa anaondoka na Sh10Milioni papo hapo kurudi nayo nyumbani huku viongozi wa benchi la ufundi na makocha wakiambulia si chini ya Sh3milioni lakini zote zilibaki stori baada ya kupoteza dabi.

Katika hatua nyingine, aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba,Barbara Gonzalez jana aliposti ujumbe kwenye akaunti za X ya Simba akionyesha kukerwa na muendelezo wa kuposti mambo yaliyopita kwenye mechi ya Yanga; “Admin, content(maudhui) ya jana zimetosha now(sasa), let’s move on(tusonge mbele). Tugange yajayo.”

SOMA NA HII  KIFO CHA KOBE BRYANT CHASIMAMISHA RATIBA YA MECHI NBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here