Home Uncategorized NAHODHA STARS ABEBA MATUMAINI YA KUTOSHA KUFUZU CHAN

NAHODHA STARS ABEBA MATUMAINI YA KUTOSHA KUFUZU CHAN


JOHN Bocco nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, amesema kuwa kwa sasa akili zao ni kwenye mchezo wa marudio dhidi ya Kenya unaotarajiwa kuchezwa Agosti 4.

Stars jana ililazimisha suluhu ya bila kufungana bao na timu ya Kenya kwenye mchezo wa kwanza wa kufunzu michuano ya Chan itakayofanyika 2020 Cameroon mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.

Bocco amesema:”Wao wameweza kupata sare nyumbani kwetu nasi tunakwenda kushinda kwao ni suala la muda na kujipanga tu hivyo mashabiki watupe sapoti kwa ajili ya kufikia malengo yetu ambayo ni kufuzu Chan,” amesema.

SOMA NA HII  LAMPARD, CHELSEA KIMEELEWEKA