Home Habari za michezo KELVIN YONDANI AMPIGIA SALUTI MSHAMBULIAJI YANGA…AMEZUNGUMZA HAYA

KELVIN YONDANI AMPIGIA SALUTI MSHAMBULIAJI YANGA…AMEZUNGUMZA HAYA

KELVIN YONDANI AMPIGIA SALUT MSHAMBULIAJI YANGA...AMEZUNGUMZA HAYA

BAADA ya kupata nafasi ya kucheza mara mbili na mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, nahodha wa zamani wa timu hiyo anayekipiga kwa sasa Geita Gold, Kelvin Yondani amekiri chipukizi huyo ni mtu sana, lakini akimtaka abadilike ili aweze kufika mbali zaidi.

Yondani, amecheza mechi mbili na mshambuliaji huyo akianza mechi ya duru la pili la Ligi Kuu Bara na juzi wamekutana tena kwenye robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), huku Geita ikipoteza zote mbele ya Yanga.

Akizungumza na SOKA LA BONGO, Yondani aliyewahi kukipiga Simba na Taifa Stars alisema Mzize ni bonge la mshambuliaji, lakini anatumia zaidi nguvu kuliko akili kitu ambacho kama atajirekebisha basi atakuwa mrithi sahihi wa John Bocco kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kati tegemeo kwa taifa.

β€œNi mchezaji mzuri nimepata nafasi ya kuzungumza naye kwani ni mchezaji ambaye amekiri ilikuwa ni ndoto yake kuona anacheza pamoja nami, hivyo tulipata wasaa wa kukaa na kuzungumza,” alisema Yondani na kuongeza;

β€œNimemwambia aendelee kupambana kutokana na nafasi anayopata mbele ya kikosi bora cha Yanga ya sasa asipoteze nafasi na nimemweleza mpira ni akili na sio nguvu yeye nichezaji mzuri na ana umbo zuri kwa nafasi anayocheza.”

Hadi sasa straika huyo chipukizi aliyepanda Yanga kubwa kutoka kikosi cha vijana ana mabao sita kwenye Kombe la ASFC na akiwa na mengine manne ya Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  MANARA ATUPA DONGO HILI JIPYA SIMBA...ADAI KILA 'MBWA' HUMJUA BOSS WAKE...